Wapiga kura milioni waliosajiliwa 24.4 wanatarajiwa kushiriki katika zoezi la kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu nchini Algeria siku ya Jumamosi, huku Rais Abdelmadjid Tebboune,aliye na umri wa miaka 78 akitarajiwa kushinda muhula wa pili wa miaka mitano afisini.
Rais Tebboune wa chama cha National Liberation Front anapingwa na Abdelaali Hassani Cherif aliye na umri wa miaka 57 na Youcef Aouchiche, mwenye umri wa miaka 41.
Idadi ndogo ya wapiga kura imejitokeza kupiga kura, huku vituo vingi vya kupigia kura vikishuhudia foleni fupi kinyume na uchaguzi wa mwaka 2019.
Taifa hilo la kaskanini mwa Afrika na kubwa zaidi linaandaa uchaguzi huku likikumbwa na misukosuko mingi ikiwemo mfumo wa juu wa bei za bidhaa.
Idadi ya wapiga kura kwenye uchaguzi wa mkuu wa mwaka huu inatarajiwa kuwa chini ya asilimi 40 ya walioshiriki uchaguzi wa mwaka 2019.