Home Burudani Akothee kupatia watoto 30 msaada wa masomo

Akothee kupatia watoto 30 msaada wa masomo

0

Mwanamuziki Esther Akoth Kokeyo maarufu kama Akothee ametangaza kwamba atatoa msaada wa masomo kwa watoto 30 kutoka familia maskini anapofungua shule yake.

Alichapisha picha za jengo la shule hiyo ya chekechea kwa jina “Akothee Academy” ambayo anasema iko karibu na mahali ambapo amejenga makazi yake ya kustaafu, huko Rakwaro kaunti ya Migori.

Akothee alielezea kwamba ufadhili wa masomo ya watoto hao utatokana na wakfu wake.

Disemba 10, 2023 ndiyo siku mwimbaji huyo alizindua rasmi shule hiyo huku akisherehekea kuhitimu kwake kutoka chuo kikuu.

Alionyesha watoto ambao meshasajiliwa tayari kwa masomo kuanzia Januari mwakani wakiwa wamevaa sare rasmi ya shule hiyo.

Mkewe aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga, Mama Ida Odinga ndiye aliongoza uzinduzi huo akiwa ameandamana na wageni kadhaa wa heshima kama mke wa Gavana wa kaunti ya Kisumu, Dorothy Nyong’o.

Shule hiyo inaanza na madarasa ya chekechea ambayo ni Kindergarten, PP1 na PP2.

“Ninataka kuhakikishia kina mama wa eneo hili mahali salama pa kuacha watoto wao wanapokwenda kujitafutia riziki kila siku.” Aliandika Akothee.

Website | + posts