Home Habari Kuu Ajira ughaibuni, Waziri Bore mawindoni

Ajira ughaibuni, Waziri Bore mawindoni

0

Waziri wa Leba Florence Bore ameimarisha jitihada za kuwatafutia vijana wa humu nchini ajira katika mataifa ya kigeni. 

Ukosefu wa ajira umetajwa kuwa swala nyeti humu nchini, na umechangia vijana wengi kujiingiza katika maovu ya kila aina ikiwa ni pamoja na uhalifu na utumiaji wa mihadarati.

Baada ya kufanikiwa kutafuta nafasi za ajira katika nchi ya Saudi Arabia ambako maelfu ya wauguzi kutoka humu nchini watapelekwa kuhudumu, Waziri Bore sasa ameelekea nchini Australia.

Kule, amekutana na Balozi wa Kenya nchini humo Dkt. Wilson Kogo.

“Tulizungumzia fursa zilizopo za ajira kwa ajili ya vijana wetu na njia bora ya kutumia vilivyo fursa zilizopo kwa sasa nchini Australia,” alisema Bore baada ya mkutano kati yake na Dkt. Kogo.

Humu nchini, serikali ya Kenya Kwanza inatumai mipango kama vile ujenzi wa nyumba za gharama nafuu itasaidia kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira.

 

Website | + posts