Home Kaunti Ajira Digital yanufaisha vijana Turkana na wakimbizi wa Kakuma

Ajira Digital yanufaisha vijana Turkana na wakimbizi wa Kakuma

0

Mpango wa ajira mitandaoni almaarufu Ajira Digital, umefika katika kaunti ya Turkana ambapo unafaidi vijana wa jamii ya eneo hilo na wakimbizi wanaoishi katika kambi ya Kakuma.

Vijana kutoka kambi hiyo ya Kakuma na wa jamii za eneo hilo hufika kwenye kituo cha dijitali cha eneo bunge la Turkana Magharibi kupokea mafunzo kuhusu jinsi ya kutekeleza kazi mbali mbali mitandaoni.

Mpango huo ni muhimu hasa kwa vijana ambao wamekamilisha masomo lakini wamekosa nafasi za ajira na utawasaidia kujipatia mapato.

Meneja wa kituo hicho Josphat Emuria anasema kufikia sasa wametoa mafunzo kwa vijana zaidi ya mia mbili kuhusu kufanya kazi za ughaibuni kupitia mtandao na pia kunadi bidhaa mtandaoni.

Bayosandra Leah ambaye ni mmoja wa walionufaika na mafunzo hayo na ambaye ni mkimbizi kutoka Uganda anasema sasa anajipatia shilingi elfu 3 kila wiki akifanya kazi mtandaoni.

Wito umetolewa kwa vijana kutumia fursa ya uwepo wa kituo hicho na kujitokeza ili wapate ujuzi utakaowasaidia badaye kwani hakuna karo inayotozwa.

Website | + posts