Home Taifa Ahmed Abdullahi achaguliwa mwenyekiti mpya wa Baraza la Magavana

Ahmed Abdullahi achaguliwa mwenyekiti mpya wa Baraza la Magavana

0
Ahmed Abdullahi - Gavana wa Wajir
kra

Gavana wa Wajir Ahmed Abdullahi ndiye mwenyekiti mpya wa Baraza la Magavana (CoG). 

Hadi kuchaguliwa kwake leo Jumatatu, Abdullahi amekuwa Naibu Mwenyekiti wa baraza hilo.

kra

Katika mkutano wa kawaida wa CoG uliofanyika katika hoteli moja jijini Nairobi, Gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga amechaguliwa kuwa Naibu Mwenyekiti wa baraza hilo.

Wadhifa wa mwenyekiti wa CoG umekuwa ukishikiliwa na Gavana wa kaunti ya Kirinyaga Anne Waiguru ambaye amehudumu kwa kipindi cha mihula miwili.

Waiguru alichaguliwa kwenye wadhifa huo mara ya kwanza mnamo mwaka wa 2022.

Wengine waliowania kuongoza baraza hilo ni Gavana wa Nyeri ambaye sasa amechaguliwa kuwa Naibu Mwenyekiti na Magavana  Muthomi Njuki (Tharaka Nithi), Joseph Ole Lenku (Kajiado) na Johnson Sakaja (Nairobi).

 

Website | + posts