Home Michezo Ahly wazuru Tunisia wakiwinda kombe la 11 la Ligi ya Mabingwa...

Ahly wazuru Tunisia wakiwinda kombe la 11 la Ligi ya Mabingwa dhidi ya Esperance

0

Al Ahly watachuana na Eserance ya Tunisia katika duru ya kwanza ya fainali kuwania taji ya ligi ya Mabingwa barani Afrika Jumamosi usiku mjini Tunis.

Ahly ambao pia ni mabingwa watetezi wanalenga taji ya 11 huku Esperance wakiwinda taji ya tano.

Katika nusu fainali vigogo hao wa Misri waliwazabua Toupiza Mazembe kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo mabao 3-0, huku Esperance wakiibwaga Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini magoli 2 bila jibu.

Ahly watakuwa wakicheza fainali ya 6 katika makala saba yaliyopita huku Esperance ikishiriki fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2009 walipotwaa ubingwa dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco.

Itakuwa fainali ya 14 kwa Ahly huku wenyeji wakishiriki kwa mara ya 8.

Ahly wameshinda mechi tatu huku Esperance wakidedea mara mbili katika mechi tano za awali.

Website | + posts