Home Habari Kuu Agnes Kalekye ateuliwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la KBC

Agnes Kalekye ateuliwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la KBC

0

Waziri wa habari, Mawasiliano na uchumi wa digitali Eliud Owalo, leo Ijumaa amemteua Agnes Kalekye Nguna kuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la utangazaji nchini KBC.

Uteuzi wa Kalekye utakaotekelezwa mara moja, utadumu kwa muda wa miaka mitatu.

Kabla ya uteuzi wake kwa wadhifa huo, Kalekye alikuwa afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Radio Afrika, na pia mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa vyombo vya habari nchini.

Kalekye anachukua mahala pa Dkt. Naim Bilal ambaye muda wake wa kuhudumu ulikamilika.