Home Habari Kuu Agizo lililozuia utekelezaji wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2023 laondolewa

Agizo lililozuia utekelezaji wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2023 laondolewa

0
Nancy Kigunzu kuzuiliwa kwa siku tano zaidi.

Mahakama ya Rufaa imeondoa agizo lililozuia utekelezaji wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2023.

Agizo hilo lilikuwa limewekwa na Mahakama Kuu.

Hata hivyo, Mahakama ya Rufaa katika uamuzi wake ilisema serikali ambayo ilikataa rufaa dhidi ya agizo hilo kupitia Waziri wa Fedha Prof. Njuguna Ndungu, imetimiza kanuni mbili za kuridhia ombi lililotakiwa.

Majaji Mohamed Warsame, Kathurima M’Inoti na Hello Omondi walikuwa wametenga tarehe ya kutolewa kwa uamuzi huo baada ya Prof. Ndung’u kusema agizo la Mahakama Kuu lilikuwa linaathiri shughuli za serikali.

Waziri aliiambia mahakama kuwa kutakuwa na janga la bajeti ikiwa agizo hilo halitaondolewa.

Mahakama ilisema kutakuwa na athari kubwa za kiuchumi ikiwa ombi la kuondolewa kwa agizo hilo halitatolewa.

Majaji hao watatu walisema rufaa hiyo itasikilizwa na kuamuliwa ndani ya siku 60.

Jaji Mkuu Martha Koome tayari ameteua jopo la majaji watatu kusikiliza kesi inayopinga kutekelezwa kwa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2023 iliyowasilishwa na Seneta wa Busia Okiya Omtatah.

Majaji wa jopo hilo ni David Majanja, Lawrence Mogambi na Christine Meoli.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here