Home Taifa Afueni kwa Sudi baada ya kushinda kesi ya vyeti ghushi

Afueni kwa Sudi baada ya kushinda kesi ya vyeti ghushi

0

Mahakama ya Nairobi leo ijumaa imetupilia mbali kesi ya vyeti ghushi iliyokuwa ikimponza mjumbe wa Kapsaret Oscar Sudi.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkuu Felix Kombo alisema kuwa mwendesha mashtaka alishindwa kuwasilisha vyeti ghushi alivyodai kuwa Sudi alimiliki huku akimkosoa kwa jinsi alivyopata baadhi ya ushahidi aliowasilisha.

Mbunge huyo wa chama tawala cha UDA alishtakiwa na Tume ya Maadili na Kupambana Ufisadi nchini, EACC kwa makosa ya kutoa maelezo ya uongo kuhusu elimu yake kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka – lEBC nchini kwa lengo la kuwania ubunge wa Kapseret mwaka wa 2013 ambao alishinda.

Vile vile, alikuwa ameshtakiwa kwa kosa la kumdanganya afisa wa EACC Derrick Kaisha katika hoteli ya Haron Court mwaka wa 2015 kuhusiana na kesi iliyomkabili.

Baadhi ya vyeti alivyotuhumiwa kughushi, ni stashahada ya usimamizi wa biashara kutoka Taasisi ya Usimamizi ya Kenya, KIM.

Boniface Musotsi
+ posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here