Home Habari Kuu Afrika Kusini kuunda serikali ya muungano wa kitaifa

Afrika Kusini kuunda serikali ya muungano wa kitaifa

0
kra

Afrika Kusini italazimika kuunda serikali ya muungano wa kitaifa, baada ya matokeo ya kura yaliyotangazwa Jumapili,kuashiria kuwa hakuna chama kilichopata uungwaji mkono inavyohitajika kikatiba ili kubuni serikali.

Asilimia 58.6 ya wapiga kura walishiriki zoezi hilo wiki jana huku chama tawala cha ANC kikipata asilimia 40.18 pekee ya kura zote.

kra

Hii ina maana kuwa chama cha ANC kinachoongozwa na Rais Cyril Ramaphosa ,kitalazimika kuunda serikali ya muungano na chama cha upinzani cha Democratic Alliance-DA au vyama vingine muradi awe na zaidi ya nusu ya viti bungeni.

Kulingana na wadadisi wa siasa nchini humo Ramaphosa atalazimika kuunda muungano na aidha chamma cha DA au vyama vingine vidogo ilimuradi awe na zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa.

Chama cha ANC kilizoa viti 159 vya ubunge katika bunge lenye idadi ya wajumbe 400 kutoka 230 kilichopata katika muhula wa kwanza chini ya Rais Ramaphosa,wakati DA kikiongeza wajumbe wake hadi 87

Vyama vinne vilishiriki uchaguzi huo wa Urais wwiki jana huku chama cah MK kikipata wabunge 58 nacho EFF kikapata wabunge 39.

Iwapo Ramaphosa akataa kuunda serikali ya muungano basi atalazimika kujiuzulu.

Kwenye matokeo rasmi ya za Urais ANC ilipata kura 6,459,683 sawa na asilimia 40.18 kikifuatwa na chama cha DA kwa kura 3,505,735 ikiwa asilimia 21.81 ya kura nacho M.K kikachukau nafasi ya tatu kwa kura 2,344,309 sawia na asilimia 14.58.

Chama cha EFF kilichukua nafasi ya nne kwa kura 1,529,961 ikiwa asilimia 9.52.

Website | + posts