Mataifa ya Afrika yangali yanasuasua siku tano tangu kuanza kwa makala ya 33 ya Michezo ya Olimpiki jijini Paris, Ufaransa.
Hadi leo Jumatatu, hakuna nchi yoyote ya bara hili iliyojishindia medali ya dhahabu.
Tunisia ndio nchi bora ikiwa ya 16 kwenye msimamo wa nishani kwa fedha moja iliyonyakuwa na Ferjani Fares katika mchezo wa Kitara au Fencing.
Misri pia imezoa shaba ya Kitara huku Afrika Kusini wakiwa na shaba waliyonyakua katika raga ya awanaume saba upande.
Waakilishi wa bara Asia Japan na Korea Kusini wanaongoza jedwali kwa medali 7, dhahabu 4,fedha 2 na shaba 1, wakifuatwa na Australia walio na dhahabu 4 na fedha 2.
Marekani ni ya nne kwa dhahabu 3 fedha 6 na shaba 3, huku wenyeji Ufaransa wakihitimisha tano bora kwa dhahabu 3,fedha 3 na shaba 2.
Timu ya Sudan Kusini ya wanaume katika Mpira wa Kikapu iliandikisha historia kurekodi ushindi wa kwanza wa Olimpiki walipotoka nyuma na kuwashinda Puerto Rico 90-79, katika kundi C ,ikiwa nchi ya kwanza ya Afrika kushinda mchuano katika Olimpiki .
Nchi nyingi za Afrika zinatarajiwa kuanza kunyakua medali za dhahabu za Olimpiki punde riadha itakapoanza Agosti 1.