Home Kimataifa Afrika inaunda wakati muhimu mmoja baada ya mwingine wa ‘Dunia ya Kusini’

Afrika inaunda wakati muhimu mmoja baada ya mwingine wa ‘Dunia ya Kusini’

Mkutano wa 19 wa kilele wa Harakati ya Kutofungamana na Upande Wowote NAM umemalizika huku Mkutano wa 3 wa wakuu wa Nchi za Kusini ukitarajiwa kufanyika mjini Kampala, Uganda.

Huu ni wakati mwingine muhimu unaomilikiwa na “Nchi ya Kusini” unaotengenezwa na bara la Afrika baada ya Misri na Ethiopia kujiunga na kundi la BRICS na Umoja wa Afrika kujiunga na G20 mwaka 2023, mambo ambayo yameonyesha ukuaji wa Afrika.

Afrika leo ni bara lililojaa uhai na uchangamfu. Idadi ya watu inaongezeka kwa kasi ya takriban 2.3% kila mwaka na inatarajiwa kufikia bilioni 2 ifikapo 2050; ikiwa moja ya mipango muhimu ya “Ajenda ya 2063” ya Umoja wa Afrika, Eneo la Biashara Huria la Afrika AfCFTA, lililozinduliwa rasmi mapema 2021, linaonyesha kikamilifu nchi za Afrika zinadhamiria kukuza mchakato wa mwingiliano wa kiuchumi; na katika masuala ya kimataifa, nchi za Afrika pia zinashiriki kikamilifu, ikiwa ni pamoja na kuunda kikundi cha upatanishi kati ya Russia na Ukraine, na kuwa na msimamo wa pamoja juu ya masuala makuu kama vile mabadiliko ya tabianchi na mageuzi ya mashirika ya kimataifa.

Afrika inaongeza kasi yake kama nguvu mpya ya dunia, inayobeba matarajio ya pamoja ya China na nchi nyingine zinazoendelea.

Katika miaka ya hivi karibuni, kama nchi kubwa zaidi inayoendelea na moja ya “Nchi za Kusni”, China daima imekuwa “mtendaji” linapokuja suala la kukuza maendeleo ya Afrika na kuongeza sauti yake kimataifa, sio tu kwa kuandaa Maonesho ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China na Maonesho ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika ili kusaidia bidhaa za Afrika kufungua soko la China na kimataifa, bali pia ni nchi ya kwanza kuunga mkono Umoja wa Afrika kujiunga na G20.

Mwakilishi maalum wa Rais Xi Jinping wa China na naibu waziri mkuu Liu Guozhong wiki hii anaendelea kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Kusini nchini Uganda, wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amemaliza ziara yake barani Afrika, ikiwa ni desturi iliyoendelea kwa miaka 34 mfululizo ya waziri wa mambo ya nje ya China kufanya ziara ya mwaka mpya barani humo.

Hatua hizi sio tu zinaonyesha hisia za dhati za China kwamba siku zote inaifikiria Afrika na kuhangaikia mahitaji ya Afrika, bali pia inabeba wajibu wa China kama nchi kuu katika kukuza na kuboresha utawala wa kimataifa. Rais Faure Gnassingbe wa Togo alisema hivi karibuni katika mkutano wake na Waziri Wang Yi kuwa, “Togo inaishukuru China kwa kulinda haki ya Afrika katika jukwaa la kimataifa, kupinga uingiliaji wa mambo ya ndani ya Afrika, na kuchukua jukumu muhimu katika maendeleo ya amani ya Afrika. Watu wa Afrika wanahitaji rafiki kama China ambayo inasikiliza matakwa ya Afrika, na hailazimishi nia yake kwa wengine.”Kama wanachama muhimu wa “Nchi za Kusini”, kuinuka kwa nchi za Afrika ni maendeleo ya kuinuka kwa “Nchi za Kusini”. Nchi zilizoendelea za leo zinatakiwa kusikiliza sauti za nchi zinazoendelea zaidi, na hii italipa haki zaidi bara la Afrika na nchi zinazoendelea, na pia itaongeza uwezo wa jamii ya kimataifa kushirikiana katika kukabiliana na changamoto za kimataifa. Kama washirika muhimu katika kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja na kulinda haki na uadilifu wa kimataifa, China na Afrika kuungana mikono kutakuwa mfano wa kuigwa kwa nchi nyingine zinazoendelea, na hivyo kuandaa mazingira mazuri ya ushirikiano wa kimataifa.