Home Kimataifa Afrika inapaswa kujikomboa kutoka minyororo ya vikwazo vya maendeleo na umaskini

Afrika inapaswa kujikomboa kutoka minyororo ya vikwazo vya maendeleo na umaskini

0
kra

Bara la Afrika linapaswa kujikomboa kutoka kwenye taasisi za kifedha ambazo zimelilemaza kutokana na madeni.

Hii hasa wakati huu ambapo kuna rasilimali chache na mdororo wa uchumi duniani.

kra

Rais William Ruto amesema Afrika inahitaji taasisi mpya ambayo itasimamia ipasavyo fursa zake zinazochipuka.

“Taasisi hiyo inapaswa kutoa mipango ya maendeleo na sera kwa ajili ya ukuaji endelevu wa Afrika,” alisema Rais Ruto.

Aliyazungumza hayo leo Alhamisi jijini Nairobi wakati wa Mkutano Mkuu wa 39 wa kila mwaka wa Kundi la Benki ya Biashara na Maendeleo, TDB Group.

Waziri wa Fedha wa Mauritius na mwenyekiti wa TDB Group Renganaden Padayachy pamoja na Waziri wa Fedha wa Kenya Prof. Njuguna Ndung’u ni miongoni mwa waliokuwapo wakati wa hafla hiyo.

Website | + posts