Home Kimataifa Afrika inanufaika na ongezeko la watu wenye ujuzi nchini China

Afrika inanufaika na ongezeko la watu wenye ujuzi nchini China

0

Hivi karibuni, Umoja wa Mataifa ulikadiria kuwa kufikia katikati ya mwaka huu, India itaipita China na kuwa nchi yenye watu wengi zaidi duniani.

Juu ya hali hii ya kawaida ya mabadiliko ya idadi ya watu, kwenye ripoti za baadhi ya vyombo vya habari vya Magharibi, inaonekana kuwa ni shida kubwa kwa China.

Je, kupoteza hadhi ya nchi yenye watu wengi zaidi duniani kuna maana gani kwa China?Kwanza, rasilimali ya watu bado ni faida kubwa kwa China.

Takwimu zinaonyesha kuwa China ina nguvu kazi ya karibu milioni 900, na idadi ya watu wanaotimia umri wa kufanya kazi inaongezeka kwa milioni 15 kila mwaka.

Ongezeko endelevu la nguvu kazi nchini China lina athari kubwa katika uboreshaji wa tija na ukuaji wa uchumi.

Wakati huo huo, China inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kushughulikia suala la ajira.

Kuna matinki rahisi kwamba kama watunga sera wa taifa moja hawatengenezi nafasi za kutosha za ajira, idadi kubwa ya watu inaweza kuwa mzigo.

Kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia kwa mwaka 2021, kiwango cha kufanya kazi kwa watu wanaotimia umri wa kufanya kazi nchini China kilikuwa ni 68%, ambacho ni cha juu zaidi kuliko kile cha nchi nyingi zenye ukubwa wa uchumi unaofanana, kwa mfano kiwango hicho kwa Marekani kilikuwa ni 61%.

Katika miaka ya hivi karibuni, Kiwango cha ushiriki wa kazi kwa wazee nchini China pia kimeongezeka katika miaka ya hivi karibuni chini ya msukumo wa serikali.

Pili, maendeleo ya nchi hayategemei idadi ya watu tu, bali pia sifa ya watu.

Ripoti ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China ilisisitiza kwamba sayansi na teknolojia ndio nguvu kuu za uzalishaji, watu wenye ujuzi ndio rasilimali kuu, na uvumbuzi ndio msukumo mkuu.

Hivi sasa, China inahama kutoka kujipatia maendeleo kwa ustadi wa chini na uzalishaji unaohitaji nguvu kazi hadi uzalishaji wa bidhaa zenye thamani kubwa kwa kutegemea teknolojia ya hali ya juu.

Takwimu zinaonyesha kuwa kila mwaka kuna zaidi ya wanafunzi milioni 10 wanaohitimu vyuoni nchini China, na idadi ya jumla ya watu wenye elimu ya juu nchini China imepita milioni 240.

Katika miaka 20 iliyopita, China pia imeandaa wahandisi milioni 60,na kuwa nchi yenye idadi kubwa zaidi ya wahandisi duniani, ambayo inakaribia idadi ya watu wote wa Ufaransa.

Tatu, watu wenye ujuzi wa China wanachangia ushirikiano kati ya China na Afrika.

Katika ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, Rais Xi Jinping wa China alipendekeza kuwa China na Afrika zitatekeleza kwa pamoja “miradi tisa”, mojawapo ikiwa ni kujenga uwezo.

Iwe ni reli, viwanja vya ndege, bandari na vituo vya kuzalisha umeme kwa maji vilivyojengwa na makampuni ya China kote barani Afrika, au ushirikiano kati ya China na Afrika katika nyanja mpya kama vile kilimo cha kisasa na teknolojia ya kidijitali, watu wenye ujuzi wa China katika nyanja mbalimbali vinahusika.

Kwenye ushirikiano huo, wachina hao pia wamefunza idadi kubwa ya vipaji vya ndani kwa nchi za Afrika na kutambua uhamisho wa teknolojia.

Wakati huo huo, data zinaonyesha kuwa tangu 2019, China imekuwa nchi ya nje ambayo wanafunzi wa Afrika wanakuja kusoma kwa wingi zaidi.

Hii sio tu inaonyesha maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika, bali pia nguvu ya China katika uandaaji wa watu wenye ujuzi inazidi kuimarika.

Kwa sasa, China inajitahidi kutafuta maendeleo yenye ubora wa juu, na kwa uhakika kwa kutegemea idadi kubwa ya watu pekee hakuwezi kufikia lengo hilo.

Kwa hiyo, wasiwasi wa “hasara zinazotokana na idadi ya watu zinazuia China kufikia lengo la kujistawisha” hauna mantiki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here