Home Kaunti Afisi ya uhamiaji kufunguliwa kaunti ya Kericho

Afisi ya uhamiaji kufunguliwa kaunti ya Kericho

Kwa mujibu wa Bittok, afisi hiyo mpya itapunguza msongamano katika vituo vya uhamiaji vya Kisumu na Eldoret, pamoja na kuokoa muda na gharama ya kusafiri.

0
Afisi ya uhamiaji kufunguliwa kaunti ya Kericho.

Katibu katika idara ya uhamiaji Julius Julius Bittok, ametangaza kuwa serikali itafungua afisi ya uhamiaji katika mji wa Kericho.

Afisi hiyo itakayohifadhiwa katika jumba la Ardhi, itafanikisha kuleta huduma karibu na wananchi kuanzia tarehe moja mwezi Januari mwaka 2024.

“Kuanzia mwaka ujao, wakazi wa eneo la South Rift hawatasafiri tena mwendo mrefu kutafuta pasipoti pamoja na stakabadhi zingine za kusafiria,” alisema katibu huyo.

Kwa mujibu wa Bittok, afisi hiyo mpya itapunguza msongamano katika vituo vya uhamiaji vya Kisumu na Eldoret, pamoja na kuokoa muda na gharama ya kusafiri.

Alisema hati hizo muhimu zitatolewa katika muda wa wiki mbili baada ya kutuma maombi ya paspoti.

Seneta wa Kericho Aaron Cheruiyot, alipongeza hatua ya serikali ya kufungua afisi ya uhamiaji Kericho, akisema italeta huduma karibu na wananchi wanaonuia kusafiri nje ya nchi.

Website | + posts