Home Kimataifa Afisa wa polisi aliyemuua George Floyd ashambuliwa gerezani

Afisa wa polisi aliyemuua George Floyd ashambuliwa gerezani

0
Derek Chauvin alishambuliwa gerezani.

Afisa wa polisi aliyemuuwa raia wa Marekani mwenye asili ya Afrika George Floyd, ambaye kifo chake kilichochea maandamano makubwa ya kupinga ubaguzi wa rangi, amejeruhiwa vibaya akiwa gerezani.

Gazeti la Marekani la NewYork Times,  limesema kuwa Derek Chauvin alichomwa kisu siku ya Ijumaa katika jela la Tucson huko Arizona lakini amenusurika baada ya kupokea matibabu hopistalini.

Gazeti la New York Times, likiwanukuu watu wawili wanaofahamu hali hiyo.

Chauvin anatumikia vifungo tofauti kuhusiana na kifo cha Mmarekani huyo mwenye asili ya Kiafrika, ambacho kilisababisha maandamano makubwa dhidi ya ukatili wa polisi na ubaguzi wa rangi.

Ofisi ya Magereza ilithibitisha katika taarifa kwamba mfungwa wa gereza hilo la jiji la Tucson alichomwa kisu saa 12.30 saa za nyumbani (19:30 GMT) siku ya Ijumaa.

Kifo cha George Floyd kilichotokea tarehe tano mwezi Mei mwaka 2020, kilisababisha maandamano makubwa dhidi ya ubaguzi wa rangi na ghasia za polisi kote nchini Marekani na sehemu mbalimbali duniani.

Website | + posts