Home Kaunti Afisa wa polisi afariki baada ya kugongwa na gari Teso Kaskazini

Afisa wa polisi afariki baada ya kugongwa na gari Teso Kaskazini

0

Afisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Amagoro, alifariki baada ya kugongwa na gari katika kizuizi cha barabarani katika barabara ya Malaba-Bungoma kaunti ndogo ya Teso Kaskazini.

Akithibitisha kisa hicho, kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Teso Kaskazini Joseph Matiku, alisema uchunguzi umeanzishwa ili kumfungulia mashtaka dereva wa gari hilo.

Kulingana na walioshuhudia kisa hicho, dereva wa gari hilo linaloaminika lilikuwa likisafirisha bidhaa za magendo, alikaidi agizo la kumtaka asimamishe gari, lakini alitoroka na kumgonga konstabo wa polisi Nancy Chepchumba.

Gari hilo lilitoroka kutoka Bungoma kuelekea katika mpaka wa Malaba.

Afisa huyo wa polisi alipelekwa katika hospitali ya Kocholia, ambako madaktari walitanga kuwa amefariki.

Tukio hilo linajiri wiki mbili tu baada ya tukio sawa na hilo kutokea , ambapo konstabo wa polisi Simiyu, aligongwa na gari katika eneo hilo hilo na kufariki alipkuwa akipokea matibabu katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya Moi.

Visa vya ajali za barabarani vimeongezeka katika barabara ya Malaba-Bungoma, huku vikichangiwa zaidi na waendeshaji pikipiki na madereva wa malori ya masafa marefu.

Website | + posts