Afisa wa jeshi wa Marekani afungwa jela kwa kuwa jasusi wa China

Tom Mathinji, BBC, BBC and BBC
1 Min Read

Afisa wa jeshi la wanamaji wa Marekani aliyekiri kutoa taarifa nyeti za kijeshi kwa China amefungwa jela kwa zaidi ya miaka miwili.

Wenheng Zhao, mwenye umri wa miaka 26, alikiri hatia mwezi Oktoba kwa kupeana taarifa kwa majasusi wa China kwa rushwa.

Zhao alikuwa afisa mdogo anayefanya kazi katika kituo cha wanamaji cha California.

Alipitisha habari kuhusu mazoezi ya kijeshi, maagizo ya operesheni na miundombinu muhimu Kuanzia 2021 hadi 2023, maafisa wa Amerika walisema.

Hasa, alitoa taarifa kuhusu mazoezi makubwa ya jeshila Wanamaji la Marekani katika eneo la Indo-Pacific, pamoja na michoro ya umeme na michoro ya mfumo wa rada ulioko kwenye kambi ya Marekani kwenye kisiwa cha Japan cha Okinawa.

Kambi ya Jeshi la Wanamaji la Marekani huko Okinawa ni muhimu kwa shughuli zake barani Asia

Website |  + posts
Share This Article