Home Kaunti Afisa mkuu mtendaji wa KEMSA Andrew Mulwa ashinda tuzo ya usimamizi bora...

Afisa mkuu mtendaji wa KEMSA Andrew Mulwa ashinda tuzo ya usimamizi bora Afrika

Tuzo hiyo, inatumiwa kutambua na kusherehekea usimamizi bora kisiasa, kijamii na kiuchumi kote barani Afrika.

0

Afisa mkuu mtendaji wa hamashauri ya usambazaji dawa nchini (KEMSA) Dkt. Andrew Mulwa, ameshinda tuzo ya usimamizi bora barani Afrika ya African Governance Award mwaka 2024.

Tuzo hiyo ilitolewa kwa Mulwa kufuatia usimamizi wake bora na uongozi wa kupigiwa mfano kama kiongozi aliyebobea barani afrika kufuatia juhudi zake kuleta mabadiliko katika halmashauri ya KEMSA.

Tuzo hiyo ambayo iliwavutia washiriki kutoka kote barani Afrika, inatumiwa kutambua na kusherehekea usimamizi bora kisiasa, kijamii na kiuchumi kote barani afrika.

Tuzo hiyo haijatambua tu ufanisi wake bali pia hadhi ya halmashauri ya KEMSA kama halmashauri ya kipekee ya usambazaji dawa barani afrika.

Dkt. Mulwa aliteuliwa afisa mkuu mtendaji wa KEMSA mwezi Mei mwaka jana na kufikia sasa uongozi wake umedhihirika kupitia tuzo hiyo iliyotambua halmashauri hiyo kama yenye usimamizi bora barani Afrika.

Website | + posts