Home Habari Kuu Afisa bandia wa tume ya EACC akamatwa

Afisa bandia wa tume ya EACC akamatwa

Mshukiwa huyo kwa jina Militonic Mwendwa Kitute, aliandamwa na maafisa hao kutoka Jijini Nairobi, hadi katika makazi yake kaunti ya Kitui, alikotiwa nguvuni.

0
Militonic Mwendwa Kitute, akamatwa kwa kujisingizia kuwa afisa wa tume ya EACC.

Maafisa wa tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi EACC, wamemkamata mshukiwa anayewahadaa wakenya kwa kujisingizia kuwa afisa wa tume hiyo.

Mshukiwa huyo kwa jina Militonic Mwendwa Kitute, aliandamwa na maafisa hao kutoka Jijini Nairobi, hadi katika makazi yake kaunti ya Kitui, alikotiwa nguvuni.

Bastola yake na simu saba za rununu ni miongoni mwa vifaa ambavyo vilitwaliwa na maafisa hao.

Mshukiwa huyo ambaye aliwania kiti cha ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022, kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kilimani.

“Mhalifu hatari na ambaye amejihami aliyewahadaa wakenya kwa kujisingizia kuwa afisa wa tume ya EACC na ambaye amekuwa akitoa vyeti ghushi vya maadili kwa wanaotafuta ajira, amekamatwa,” ilisema taarifa ya EACC.

Baadaye mshukiwa huyo alipelekwa katika mahakama za milimani.

Website | + posts