Home Michezo AFCON 2025: Kenya kuchuana na Namibia Jumanne usiku

AFCON 2025: Kenya kuchuana na Namibia Jumanne usiku

Mchuano huo utaandaliwa mjini Orlando, Soweto Afrika Kusini.

0
kra

Timu ya taifa ya soka Harambee Stars itachuana na Namibia leo Jumanne saa moja usiku, katika mechi ya Kundi J kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2025.

Mchuano huo utaandaliwa mjini Orlando, Soweto Afrika Kusini.

kra

Stars inayofunzwa na kocha Engin Firat, ilitoka sare tasa na Zimbabwe juma lililopita nchini Uganda, na inalenga kuboresha matokeo hayo itakapokutana na Namibia.

Kenya na Zimbabwe zinashikilia nafasi ya pili kwa alama moja nayo Namibia inavuta mkia bila alama.

Katika kundi hilo, mabingwa mara tano wa Afrika Cameroon,  wanaongoza kundi hilo la J wakiwa na alama tatu baada ya kuifunga Namibia katika mechi yao ya ufunguzi Ijumaa iliyopita.

Kenya na Namibia zimekutana mara sita awali na zilikutana mara ya mwisho mwaka 2013 wakati wa mchujo wa kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia 2014 ambapo Kenya iliifunga bao 1-0.

Timu mbili bora katika kila kundi zitafuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka ujao jijini Rabat, Morocco.

Website | + posts