Timu ya taifa ya soka Harambee Stars ilifufua matumaini yake ya kufuzu kwa michuano ya Mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2025, baada ya kuilaza Namibia 2-1 Jumanne usiku.
Stars walipata bao la kwanza kupitia mchezaji John Avire katika dakika ya 57, kabla ya Duke Abuya kufunga la pili katika dakika ya 77.
Aidha Namibia walijikakamua lakini juhudi zao ziliwapatia bao la kufuta machozi katika dakika za mwisho mwisho kupitia mchezaji Dione Hotto.
Ushindi huo umeiweka Stars kileleni pa jundi hilo ikiwa na alama nne sawa na mabingwa wa Afrika mara tano Cameroon,lakini Kenya inaongoza kwa wingi wa mabao.
Mechi hiyo ilichezwa katika uwanja wa Orlando, Jijini Johanesburg, Afrika Kusini.
Kocha mkuu wa Harambee Stars Engin Firat, aliwapongeza wachezaji wake kwa kuzingatia mawaidha yake wakati wa mchuano huo.
“Tunataka kushinda mechi zilizo salia ili kudumisha matumaini yetu ya kufuzu,” alisema Firat.
KatikaJedwali hilo, Zimbabwe ni ya pili ilihali Namibia inavuta mkia bila alama.