Mji wa Addis Ababa nchini Ethiopia umeteuliwa kuandaa kikao cha kawaida cha 46 cha Shirikisho la Soka barani Afrika, CAF tarehe 22 mwezi ujao.
Itakuwa ni mara ya kwanza kwa Ethiopia kuandaa kikao hicho.
Kenya pia ilitunukiwa maandalizi ya kikao cha Baraza Kuu la CAF Septemba 16 mwaka huu kilichoongozwa na Rais Dkt. Patrice Motsepe.