Home Biashara AA yalenga wanachama milioni 20 katika ushirikiano na kampuni za bima

AA yalenga wanachama milioni 20 katika ushirikiano na kampuni za bima

0

Kampuni ya AA Kenya imeongeza ushirikiano na kampuni za bima ili kupendekezea wateja mazuri yanayotokana na uanachama wa AA.

Katika kujitolea kwake kusaidia wamiliki na waendeshaji magari kote nchini, kampuni ya AA Kenya sasa inashirikiana na kampuni za bima ambazo zitawapatia wenye magari malipo mazuri kugharimia mahitaji yao tofauti.

Wamiliki wa magari sasa wanaweza kujisajili kama wanachama wa AA wakati wanalipia bima huku AA ikilenga kusajili Wakenya milioni 20.

Kuna viwango tofauti vya uanachama wa AA ambavyo vinawawezesha kupata mafunzo ya bure ya usalama barabarani, usaidizi barabarani, kupata punguzo la bei kutoka kwa washirika wa AA kwa huduma za kuburura magari kati ya huduma nyingine.

Kiwango cha wamiliki wa magari kinafahamika kama Signature huku cha wasio wamiliki au waendeshaji magari kikifahamika kama Champion.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo wa ushirikiano, Mkurugenzi Mtendaji wa AA Francis Theuri alisema watu ambao wana ujuzi watadumisha usalama barabarani.

Kwa sababu hiyo, Theuri alisema mafunzo, kuhusisha umma na utetezi ni nguzo muhimu kwenye mipango ya AA ya kuhakikisha usalama barabarani.

Kando na faida hizo, kampuni ya AA imeshirikiana na wakfu wa utafiti wa kimatibabu, AMREF kutoa huduma za ambulensi za ndege na magari kwa wanachama wake kwa bei iliyopunguzwa.

Kampuni ya mafuta ya Total Kenya nayo itawapa wanachama wa AA punguzo la shilingi mbili kwa kila lita ya mafuta, punguzo la hadi asilimia 25 kwa vipuri vya magari na punguzo la bei ya huduma ya kawaida ya magari.

Kila mwanachama wa AA kiwango cha Signature atakuwa analipa shilingi elfu 3 kwa kila gari kila mwaka huku wale wa kiwango cha Champin wakilipa shilingi 200 kila mwaka.

Wanachama wa kiwango cha Champion watapatiwa mafunzo ya ziada kuhusu namna ya kutumia barabara, kutumia maeneo yaliyotengewa wanaotembea kwa miguu na kutii alama za barabarani.

Lengo kuu la mpango mzima wa uanachama wa AA ni kupunguza ajali na kuhimiza utamaduni wa kutumia barabara kwa kuwajibika.

Website | + posts