Home Kaunti
0

Maziwa katika kaunti ya Nakuru ni rasilimali muhimu kwa uchumi wa majini na yanafaa kutumiwa kwa njia zifaazo ili kaunti hiyo ifikie lengo lake la kuimarisha mapato.

Kamishna wa tume ya ugavi wa mapato Hadija Juma ameupa changamoto ugatuzi utumie rasilimali ipasavyo kwenye maziwa ya Naivasha, Nakuru, Solai, Elementaita, Oloiden pamoja na kasoko ya Menengai ili kuimarisha mapato yake.

Akizungumza wakati alipoongoza ujumbe kwenye afisi ya gavana Susan Kihika, Kamishna Juma alisema kwamba miradi hiyo pamoja na shughuli kwenye maziwa zitasaidia kutoitegemea serikali ya kitaifa.

Gavana Kihika akipendekeza kujumuishwa kwa uchumi wa majini katika mfumo wa ugawaji mapato, alisikitika kwamba kaunti hiyo haikunufaika kutokana na mapato kutoka mbuga ya wanyama ya Nakuru pamoja na kawi ya jotoardhi inayozalishwa Olkaria na Menengai.

Kihika alitoa wito kwa uchapishwaji kwenye gazeti rasmi la serikali kwa ziwa Solai ili kuruhusu kutumiwa vyema kwa rasilimali zake huku kaunti ya Nakuru ikiimarisha uwezo wake wa kuanza kupokea mapato zaidi.

Miito hii inajiri wiki moja kabla ya kaunti hiyo kuadhimisha siku ya kimataifa ya utalii inayoratibiwa tarehe 27 mwezi huu kwenye ziwa la Elementaita.

Website | + posts