Home Habari Kuu 47 wajeruhiwa kwenye mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine

47 wajeruhiwa kwenye mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine

0
kra

Watu wapatao 47 wakiwemo watoto, walijeruhiwa kwenye mashambulizi ya makombora ya Urusi katika mji wa Kharkiv ambao ni wa pili kwa ukubwa kati ya miji nchini humo.

Shambulizi hili lililoanza jana Jumapili saa saba mchana saa za nchi hiyo liliathiri kituo cha kibiashara na cha michezo kwenye mji huo ulio karibu na mpaka wa Urusi.

kra

Meya wa mji huo aitwaye Ihor Terekhov alisema maeneo ya Saltivskyi na Nemyshlianskyi ndiyo yaliathiriwa sana na mashambulizi hayo huku ikiripotiwa kwamba Urusi ilitumia makombora yake aina ya Iskander.

Mtoto wa umri mdogo zaidi kati ya waliojeruhiwa ni wa miezi mitatu tu na kwamba wengi kati ya majeruhi wako katika hali mbaya.

Kulingana na Meya Terekhov, makundi ya uokoaji yanayojumuisha madaktari na ambulensi zao yaliyokuwa yakijibu dharura hiyo pia yalishambuliwa.

Mashambulizi haya yanajiri siku chache tu baada ya mengine yaliyosababisha vifo saba na kuacha watu wengi na majeraha. Silaha za Urusi ziligonga jumba la makazi la kuzua moto.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amerejelea wito wake kwa marafiki wa nchi hiyo wa magharibi kukubalia nchi yake kutumia silaha zao kushambulia Urusi.

Hatua hiyo kulingana naye itasaidia kupunguza tishio la wanajeshi wa Urusi. Alisema pia kwamba kinachohitajika sasa ni ujasiri wa viongozi kuipa Ukraine inachohitaji kujilinda.

Website | + posts