Home Michezo Usajili wa wanariadha kidijitali waanza

Usajili wa wanariadha kidijitali waanza

0
kra

Zaidi ya wanariadha na makocha 4000 kutoka Kaunti za Nandi, Uasin Gishu na Elgeyo Marakwet wanatarajiwa kusajiliwa kidijitali Kama njia moja kurahisisha huduma kwa wanariadha wote nchini.

Akizungumza wakati zoezi hilo katika uga wa Eliud Kipchoge Complex mjini Kapsabet Kaunti ya Nandi, Katibu Katika shirikisho la riadha nchini tawi la bonde la ufa Kennedy Tanui amesema usajili huo utazuia Baadhi ya Makocha ambao wana nia fiche ya kuhusisha wanariadha na dawa za kusisimua misuli.

kra

Aidha wanariadha ambao hudanganya umri wao kabla ya kushiriki mashindano mbalimbali pia wamelengwa bila huruma Katika zoezi hilo ili kuboresha hali ya michezo nchini.

Tanui alielezea kwamba kila mwanariadha atakayesajiliwa atapatiwa mkufunzi rasmi kama njia ya kuzuia aliowataja kuwa wakufunzi wafanya biashara ambao nia yao ni kuwapa wanariadha dawa zilizoharamishwa.

Kenya katika miaka ya hivi karibuni imekuwa ikikumbwa na tatizo la wanariadha kupigwa marufuku kushiriki mashindano yoyote kwa kupatikana na hatia ya kutumia dawa hizo zilizoharamishwa.

Website | + posts
Kimutai Murisha
+ posts