Home Kaunti Wavinya akosoa kuteuliwa kwa wanachama wa ODM kwa Baraza la Mawaziri

Wavinya akosoa kuteuliwa kwa wanachama wa ODM kwa Baraza la Mawaziri

0
kra

Gavana wa kaunti ya Machakos Wavinya Ndeti amekosoa hatua ya baadhi ya wanachama wa muungano wa Azimio  kupendekezwa kuhudumu katika Baraza Jipya la Mawaziri.

Wanachama wa ODM John Mbadi, Opiyo Wandayi, Ali Joho na Wycliffe Oparanya waliteuliwa na Rais William Ruto kujiunga na baraza hilo jana Jumatano.

kra

Wavinya amemshtumu kinara wa Azimio Raila Odinga kwa kutumia fursa ya juhudi za vijana wa Gen Z za kujaribu kuleta mabadiliko nchini kushawishi kufanywa kwa uteuzi huo.

Wavinya aliyasema hayo alipokagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ya kaunti hiyo.

Radio Taifa
+ posts